Mkwawa Journal of Education and Development (MJED)
UDSM Header
MJED | New Articles
New Articles in Volume No. 2, Issue No. 1 (2018)
TitleDoes going abroad benefit my country? Views of highly skilled personnel from Sub-Saharan Africa on brain drain-brain circulation , Vol. 2, Issue 1
Abstract
The debate on brain drain-brain circulation has been a long-lasting phenomenon of interest among educators in the field of education, in particular, international and comparative education. This long-lasting debate triggered us to rethink about the effects which the concept has on the source country as well as the destination country. The study explored the perceptions of Highly Skilled Personnel (HSPs) residing in Sub-Saharan Africa on HSPs mobility. Respondents for this study comprised of 43 Sub-Saharan African scholars. Data were collected into two phases. First, all the 43 respondents actively participated in a four-day Online Focused Group Discussion (OFGD) moderated by the researchers. The second phase involved online interviews with 12 members who also participated in the first phase. Findings indicated that the majority of respondents favoured brain circulation. This implies a significant shift from brain drain to brain circulation. The socio-economic and political contexts of countries where respondents came from influenced their responses. We suggest that in the current globalized world, instead of restricting HSPs mobility, Sub-Saharan African countries need to create attractive working environment as a means to retain the best talents and motivate those who left to come back. Furthermore, Sub-Saharan African countries must work with diaspora to improve knowledge and business networks that will enable these countries to improve their economies thereby compensating the cost incurred in educating mobile talents. Finally, brain drain-brain circulation agenda should not be viewed in isolation rather as multidimensional in nature due to its overarching countless influencing factors.

K/Words

Highly Skilled Personnel (HSPs); HSPs mobility; Brain drain; Brain circulation; Sub-Saharan African countries

Author

Patrick Severine Kavenuke

Uploaded

21 October 2019
Download Full Article (PDF)

TitleUwi ni Sifa ya Ujumi wa Kiafrika? Mifano kutoka Diwani ya Mnyampala, Mashairi ya Saadan na Kivuli cha Mvumo, Vol. 2, Issue 1
Abstract
Uwi ni dhana ya kiujumi inayowatatiza watu wengi kwa sababu huko nyuma ujumi ulijulikana kama uzuri. Jamii mbalimbali ulimwenguni zina aina mbalimbali za ujumi. Afrika ina aina mahsusi za ujumi ambazo hutambulishwa na vipengele anuwai katika sanaa zake. Makala hii inaangazia uthibitisho wa kuwa uwi ni sifa ya kiujumi wa Waafrika. Aidha, data zilizotumika katika makala hii zimekusanywa kwa njia ya maktaba iliyohusisha usomaji wa vitabu, makala na tasnifu. Njia hii ilitumika kwa sababu ya kupata data za upili na kubaini mapengo yaliyojitokeza katika tafiti zilizotangulia. Vitabu teuli ni vya mashairi kutoka diwani tatu ambazo ni Diwani ya Mnyampala ya Mathias Mnyampala, Mashairi ya Saadan ya Saadan Kandoro na Kivuli cha Mvumo ya Rashid Mfaume yamehusishwa kama rejea kuthibitisha kuwa uwi ni sifa ya ujumi wa Waafrika. Nadharia ya Unegritudi inayokitwa katika mikabala ya Kiafrika, ndiyo iliyoongoza mjadala wa matokeo wa makala hii. Imethibitika kuwa uwi ni kitu cha kiujumi hivyo kinapaswa kumakinikiwa kwa namna iliyo sawa na uzuri.

K/Words

Ujumi; Uwi; Waafrika; Idili

Author

Birigitha Ngwano John

Uploaded

21 October 2019
Download Full Article (PDF)

TitleKiswahili Katika Taathira ya Kihistoria na Mielekeo ya Kisiasa kama Lugha ya Kufundishia, Vol. 2, Issue 1
Abstract
Makala hii inahusu Kiswahili katika taathira ya kihistoria na mielekeo ya kisiasa kama lugha ya kufundishia elimu ya juu hapa nchini Tanzania. Makala hii inaeleza mambo yanayosababisha mielekeo tofauti ya watu kuhusu upokezi na matumizi ya lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia elimu ya juu nchini Tanzania ili kushurutisha ukubalifu wake. Baadhi ya masuala yanayochunguzwa ni yale yanayotiliwa shaka kuhusu uwezo wa lugha ya Kiswahili kumudu na kukidhi harakati za mahitaji ya kufundishia elimu ya juu, pamoja na kupitisha teknolojia mpya inayoinukia katika nyanja za sayansi na teknolojia. Aidha, makala hii inanuia kufafanua ukubalifu, pamoja na msingi wa mielekeo ya Watanzania kutoipatia kipaumbele lugha ya Kiswahili kama lugha inayoweza kukidhi mahitaji ya kufundishia elimu ya juu hapa nchini. Data za msingi katika makala hii zilipatikana maktabani kwa kudurusu nyaraka mbalimbali zilizohusiana na mada iliyolengwa. Mapitio ya nyaraka mbalimbali zilizotumika kushadidia data za msingi za mada iliyochunguzwa zilipatikana katika maktaba ya chuo kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha iliyopo Iringa. Makala hii inahitimisha kwamba lugha za kigeni na zile za kiasili zinaweza kuendelea kutumika pamoja katika ngazi zote za elimu ili kuziwezesha kutekeleza vema dhima zake.

K/Words

Taathira; Taathira ya kihistoria; Mielekeo ya kisiasa; Lugha ya kufundishia

Author

Gerephace - Mwangosi

Uploaded

21 October 2019
Download Full Article (PDF)

TitleEditorial, Vol. 2, Issue 1
Abstract
Editorial

K/Words

Editorial; MJED; Vol 2

Author

Editor - -

Uploaded

21 October 2019
Download Full Article (PDF)

Main Jquery